منتديات إنما المؤمنون إخوة (2024 - 2010) The Believers Are Brothers

(إسلامي.. ثقافي.. اجتماعي.. إعلامي.. علمي.. تاريخي.. دعوي.. تربوي.. طبي.. رياضي.. أدبي..)
 
الرئيسيةالأحداثأحدث الصورالتسجيل
(وما من كاتب إلا سيبلى ** ويبقى الدهر ما كتبت يداه) (فلا تكتب بكفك غير شيء ** يسرك في القيامة أن تراه)


IZHAR UL-HAQ

(Truth Revealed) By: Rahmatullah Kairanvi
قال الفيلسوف توماس كارليل في كتابه الأبطال عن رسول الله -صلى الله عليه وسلم-: "لقد أصبح من أكبر العار على أي فرد مُتمدين من أبناء هذا العصر؛ أن يُصْغِي إلى ما يظن من أنَّ دِينَ الإسلام كَذِبٌ، وأنَّ مُحَمَّداً -صلى الله عليه وسلم- خَدَّاعٌ مُزُوِّرٌ، وآنَ لنا أنْ نُحارب ما يُشَاعُ من مثل هذه الأقوال السَّخيفة المُخْجِلَةِ؛ فإنَّ الرِّسَالة التي أدَّاهَا ذلك الرَّسُولُ ما زالت السِّراج المُنير مُدَّةَ اثني عشر قرناً، لنحو مائتي مليون من الناس أمثالنا، خلقهم اللهُ الذي خلقنا، (وقت كتابة الفيلسوف توماس كارليل لهذا الكتاب)، إقرأ بقية كتاب الفيلسوف توماس كارليل عن سيدنا محمد -صلى الله عليه وسلم-، على هذا الرابط: محمد بن عبد الله -صلى الله عليه وسلم-.

يقول المستشرق الإسباني جان ليك في كتاب (العرب): "لا يمكن أن توصف حياة محمد بأحسن مما وصفها الله بقوله: (وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلَّا رَحْمَةً لِّلْعَالَمِين) فكان محمدٌ رحمة حقيقية، وإني أصلي عليه بلهفة وشوق".
فَضَّلَ اللهُ مِصْرَ على سائر البُلدان، كما فَضَّلَ بعض الناس على بعض والأيام والليالي بعضها على بعض، والفضلُ على ضربين: في دِينٍ أو دُنْيَا، أو فيهما جميعاً، وقد فَضَّلَ اللهُ مِصْرَ وشَهِدَ لها في كتابهِ بالكَرَمِ وعِظَم المَنزلة وذَكَرَهَا باسمها وخَصَّهَا دُونَ غيرها، وكَرَّرَ ذِكْرَهَا، وأبَانَ فضلها في آياتٍ تُتْلَى من القرآن العظيم.
(وما من كاتب إلا سيبلى ** ويبقى الدهر ما كتبت يداه) (فلا تكتب بكفك غير شيء ** يسرك في القيامة أن تراه)

المهندس حسن فتحي فيلسوف العمارة ومهندس الفقراء: هو معماري مصري بارز، من مواليد مدينة الأسكندرية، وتخرَّجَ من المُهندس خانة بجامعة فؤاد الأول، اشْتُهِرَ بطرازهِ المعماري الفريد الذي استمَدَّ مَصَادِرَهُ مِنَ العِمَارَةِ الريفية النوبية المَبنية بالطوب اللبن، ومن البيوت والقصور بالقاهرة القديمة في العصرين المملوكي والعُثماني.
رُبَّ ضَارَّةٍ نَافِعَةٍ.. فوائدُ فيروس كورونا غير المتوقعة للبشرية أنَّه لم يكن يَخطرُ على بال أحَدِنَا منذ أن ظهر وباء فيروس كورونا المُستجد، أنْ يكونَ لهذه الجائحة فوائدُ وإيجابيات ملموسة أفادَت كوكب الأرض.. فكيف حدث ذلك؟!...
تخليص الإبريز في تلخيص باريز: هو الكتاب الذي ألّفَهُ الشيخ "رفاعة رافع الطهطاوي" رائد التنوير في العصر الحديث كما يُلَقَّب، ويُمَثِّلُ هذا الكتاب علامة بارزة من علامات التاريخ الثقافي المصري والعربي الحديث.
الشيخ علي الجرجاوي (رحمه الله) قَامَ برحلةٍ إلى اليابان العام 1906م لحُضُورِ مؤتمر الأديان بطوكيو، الذي دعا إليه الإمبراطور الياباني عُلَمَاءَ الأديان لعرض عقائد دينهم على الشعب الياباني، وقد أنفق على رحلته الشَّاقَّةِ من مَالِهِ الخاص، وكان رُكُوبُ البحر وسيلته؛ مِمَّا أتَاحَ لَهُ مُشَاهَدَةَ العَدِيدِ مِنَ المُدُنِ السَّاحِلِيَّةِ في أنحاء العالم، ويُعَدُّ أوَّلَ دَاعِيَةٍ للإسلام في بلاد اليابان في العصر الحديث.


 

 FADHILA ZA MWEZI WA SHAABAN NA UZUSHI WA NISFU SHAABAN

اذهب الى الأسفل 
كاتب الموضوعرسالة
أحمد محمد لبن Ahmad.M.Lbn
مؤسس ومدير المنتدى
أحمد محمد لبن Ahmad.M.Lbn


عدد المساهمات : 52115
العمر : 72

FADHILA ZA MWEZI WA SHAABAN NA UZUSHI WA NISFU SHAABAN Empty
مُساهمةموضوع: FADHILA ZA MWEZI WA SHAABAN NA UZUSHI WA NISFU SHAABAN   FADHILA ZA MWEZI WA SHAABAN NA UZUSHI WA NISFU SHAABAN Emptyالسبت 21 أبريل 2018, 5:55 am

بسم الله الرحمن الرحيم
FADHILA ZA MWEZI WA SHAABAN NA UZUSHI WA NISFU SHAABAN Sha0n10
FADHILA ZA MWEZI WA SHAABAN
NA UZUSHI WA NISFU SHAABAN
Imeandaliwa na: Yunus Kanuni Ngenda
Imepitiwa na: Abubakari Shabani Rukonkwa
FADHILA ZA MWEZI WA SHAABAN NA UZUSHI WA NISFU SHAABAN Ao_uu11
Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu Mola wa viumbe vyote, na rehma na amani zimwendee Mtume wetu Muhammad (s.a.w) na watu wake na Maswahaba wake wote. Amma baad:

Mwezi wa Shaaban ni mwezi wa nane katika kalenda ya Kiislam. Na ni mwezi ambao upo katikati ya miezi miwili mitukufu; Rajab na Ramadhaan. Mambo ya kuzingatia katika mwezi huu ni kuweza kupambanua yaliyo sahihi na yaliyozushwa, kwani ingawa kuna fadhila zake mwezi huu lakini pia mengi yaliyoenea na yanayofanywa na watu, ni ya Upotofu.

Ni mwezi ambao Mtume )S.a.w) alikuwa akifunga sana Swawm za Sunnah kama ilivyothibiti katika Hadiyth ifuatayo kutoka kwa Mama wa Waumini ‘Aaishah (R.a) “Mtume (S.a.w) alikuwa akifunga hadi tukadhani kuwa hatofungua kamwe, na alikuwa akiacha kufunga hadi tukadhani hatofunga tena. Sijamuona Mtume (S.a.w) akifunga mwezi mzima kama alivyokuwa akifunga Ramadhaan, na sijamuona akifunga mara nyingi kama alivyofunga katika Sha’abaan” [Al-Bukhaariy na Muslim].

SWAUMU NA FADHILA ZA MWEZI WA SHAABAN:
Juu ya kwamba Mtume (S.a.w) alikuwa akifunga mara nyingi zaidi katika mwezi wa Sha’abaan kuliko miezi mingine ukiondosha Ramadhaan, kama ambao unafungwa wote, hakuwahi hata mara moja kuufunga mwezi mzima wa Sha’abaan. Na ni jambo ambalo lenye kuchukiza kufanya hivyo kama wanavyotueleza wanachuoni kama kina Ibnul Mubaarak na wengi wengine, pia Swahaba mtukufu Ibn ‘Abbaas anasema ni makruhu kufunga mwezi mzima wa Sha’abaan kwani Mtume wa Allah hakufanya hivyo.

Imepokewa kuwa Ibn ‘Abbaas (R.a) amesema: ‘‘Mtume wa Allaah (S.a.w) hakuwahi kufunga mwezi wowote kikamilifu isipokuwa Ramadhaan.
[Al-Bukhaariy].

Kukithirisha kwake Mtume (S.a.w) ibada katika mwezi huu wa Sha'abaan, ni kutokana na maelezo yake mwenyewe alipoulizwa na Usaamah bin Zayd (R.a) sababu ya kufunga sana katika mwezi huu alijibu:“[Sha'abaan] ni mwezi ambao watu hawautilii sana maanani, ulio kati (ya miezi miwili mitakatifu) Rajab na Ramadhaan, na ni mwezi ambao matendo yanapandishwa kwa Mola wa ulimwengu. Nami napenda matendo yangu yapandishwe na hali nikiwa nimefunga” [An Nasaaiy, at-Targhiyb wat-Tarhiyb, uk. 425].

Kufunga katika mwezi wa Shaaban ni mazoezi kabla ya Ramadhaan. Hata hivyo, kufunga mwezi mzima wa Sha'abaan ni Makruhu (hakupendezi) na ni kinyume na Sunnah za Mjumbe wa Allaah (S.a.w).

Ibn 'Abbaas (R.a) amesema:“Msiutangulie Ramadhaan kwa (kufunga) siku moja au mbili, ila kwa wale tu wenye mazoea ya kufunga kila mara, na kwa hali hiyo hao wanaweza kufunga (siku hizo)” Al-Bukhaariy


JE KATIKA NISFU SHAABAN KUNA UKWELI WOWOTE NDANI YAKE?
Pamoja na ubora huo na daraja hiyo ya mwezi wa Sha'abaan, Mtume (S.a.w) hakuihusisha siku maalum katika mwezi wa Shaaban kufunga.

Alikuwa akifunga kwa wingi iwezekanavyo lakini hakutueleza na wala hakuichagua siku ya tarehe 15 ya Shaaban kufunga kutokana na sifa zake alizozitaja hapo nyuma, ila tu ametaja Fadhila za usiku huu kutokana na hadiyth hii ambayo hata hivyo haikutaja kuwa kuna ibada maalum inapaswa ifanyike siku hii au usiku wake.

Imetoka kwa Abu Muusaa Al-Ash'ariy (R.a) kwamba Mtume (S.a.w) kasema: “Allaah Mtukufu Hutokea Katika usiku wa 15 wa Shaaban, na Huwasamehe wote isipokuwa Washirikina na wale wenye uadui kwa wengine.” Ibn Maajah na imesemwa kuwa ni Hadiyth Hasan na Shaykh Al-Albaaniy.

Jambo la kushangaza ni kwamba wengi katika Waislam kwa uchache wa elimu na pia kwa kufuata mafundisho yasiyo sahihi ambayo amesingiziwa nayo Mtume (S.a.w) wameitenga siku hiyo ya Nisfu Sha'abaan kufunga na kusimama kisimamo cha usiku na kusoma nyiradi mbalimbali ambazo wamezitunga na pia kusherehekea kwa namna mbalimbali. Sehemu nyingi ulimwenguni hufanya sherehe na Swawm pamoja na kuswali sana usiku kwa kuiadhimisha siku hiyo ambayo huamini ni ya aina yake.

Kuna waliyoipa jina la Shab-E-Baraat au Laylatul Bara-at (usiku wa kuachiwa huru [na moto], au wa kusamehewa) kama huko bara Hindi, Pakistan na Bangladesh. Na kwengine hujulikana zaidi kwa Nisfu Sha'abaan n.k. ambapo katika siku hiyo wanaamini kuwa ni siku ya kusamehewa kwani Allaah Anawaachia huru waja wake walio motoni kutokana na mojawapo ya Hadiyth zisizo sahihi zilizohusishwa na mwezi huu wa Sha'abaan kama hii“Allaah Anawaachia huru waja wake walio motoni kulingana na idadi ya nywele zilizo katika ngozi za mbuzi/kondoo wa Banu Kalb.”

Vilevile kuna imani potofu kabisa katika siku hii, ambapo kuna baadhi ya watu wanaamini kuwa kushuka kwa Malaika na Ruuh usiku huo kama ilivyo katika Suratul-Qadr Aayah ya 4, wao wameelewa maana yake ni kuwa Ruuh iliyokusudiwa katika sura hiyo ni roho za wale waliokufa! Na kwamba 'roho' hizo zashushwa na kurejea duniani na kukutana na wake wa wenye hizo roho na jamaa zao wengine. Na kwa sababu hiyo, wale wajane hupika vyakula bora vilivyokuwa vikipendwa na hao waume zao waliokufa kisha huviandaa na kusubiri ziara zao kutoka huko walipo. Baadhi ya watu pia huzuru makaburi katika siku hiyo na kuwaombea msamaha wale wote waliokufa mwezi wa Shaaban uliopita na huo walio nao.

Tunamuomba Allah atupe nguvu tuweze kushikamana na Sunnah za Mtume wetu Muhammad (S.a.w) katika maisha yetu. Ameen!!


FADHILA ZA MWEZI WA SHAABAN NA UZUSHI WA NISFU SHAABAN 2013_110
الرجوع الى أعلى الصفحة اذهب الى الأسفل
https://almomenoon1.0wn0.com/
 
FADHILA ZA MWEZI WA SHAABAN NA UZUSHI WA NISFU SHAABAN
الرجوع الى أعلى الصفحة 
صفحة 1 من اصل 1
 مواضيع مماثلة
-
» Perayaan Nisfu Sya’ban )Indonesian(

صلاحيات هذا المنتدى:لاتستطيع الرد على المواضيع في هذا المنتدى
منتديات إنما المؤمنون إخوة (2024 - 2010) The Believers Are Brothers :: (English) :: Famous months and days :: Shaaban-
انتقل الى: